Luke 2:10-12

10 aLakini malaika akawaambia: “Msiogope. Kwa maana tazama nawaletea habari njema za furaha itakayokuwa kwa watu wote. 11 bLeo katika mji wa Daudi kwa ajili yenu amezaliwa Mwokozi, ndiye Al-Masihi
Al-Masihi maana yake ni Masiya , yaani Aliyetiwa mafuta.
Bwana.
12 dHii ndiyo itakayokuwa ishara kwenu: Mtamkuta mtoto mchanga amefunikwa nguo za kitoto na kulazwa katika hori ya kulia ng’ombe.”

Copyright information for SwhKC